ZIGGY MARLEY AMEFUNGUKA MPANGO WA KUTENGENEZA FILAMU YA MAISHA BOB MARLEY


Mtoto wa kwanza wa The Late Reggae Legend Bob Marley, Ziggy Marley amefunguka mpango wake wa kuileta filamu ya Maisha (biopic) ya nguli huyo.
Imeripotiwa kuwa, Ziggy ameshirikiana na kampuni ya kutengeneza filamu nchini Marekani, Paramount Pictures kuiandaa filamu hiyo ambayo itazungumzia maisha ya Nguli huyo wa Muziki wa Reggae, kuanzia Hustling zake kwenye Mitaa ya Jamaica mpaka kuwa Kioo cha dunia kwenye miaka ya 1970.
Bado haijawekwa wazi kuwa ni nani atacheza Uhusika wa Bob Marley, na lini itatoka. | Bob alifariki dunia mwaka 1981 kwa Ugonjwa wa Saratani akiwa na umri wa miaka 36.

Kizazi cha Reggae kimebaki na kumbukumbu ya Hits zake pamoja na Classic albums, zikiwemo: Catch a Fire (1973), Burnin' (1973), Rastaman Vibration (1976) na Exodus (1977), ambazo ziliuza zaidi ya nakala Milioni 75.
Post a Comment
Powered by Blogger.