@MwanaFA Featuring @MauaSama - Hata Sielewi (Official Music Video) + Lyrics

Kwa mara nyingine tena ni Mwana FA na Maua Sama kwenye  "Hata Sielewi" ngoma ambayo inazungumzia stori ya wapendanao wawili waliozama kwenye mapenzi bila kujua kilichowafanya wazame kiasi hicho.

Cheki Nayo Hapa:

  LYRICS: 

LYRICS:

Faaalsafaa
Falsafa Hommie
Samaa
Are you listening?

Verse I (MwanaFA)
Bonge la mtoto/bonge la zigo/
Naamini sioti coz naipenda hii ndoto/
Sitoi boko/na naamini hayuko soko/
Ntamvisha pete leo leo/
Sio wa mchezo ka kazi ya kwenye video/
Ananikaanga roho/ananisaga moyo/
Sipo sawa akili imevurugwa nayo/
Nilikuwa poa tu kabla hatujakutana/
Gangster kama mimi hakuna/
Hana wasiwasi anatembea kama hataki,anajivuuta/
na kila hatua ina nukta/
Kiuno cha nyigu/rangi ya kinugu/
Nashangaa maujuzi ya Mungu/
Hakuna kovu hakuna sugu/
Maswali bila ya majibu/

HOOK:
So unafanya nionekane chizi/
Hata sielewi nini la kufanya/
Akili hazifanyi ka zimekufa ganzi/
Hata sielewi naona nyota mamaa/
Where you coming from?/
Hata Sielewi/Sielewi/
Where you coming from?/
Hata Sielewi/Sielewi/

Sielewi Sielewi Eeh,Eeh
Sielewi Sielewi Eeh,Eeeh


Verse II (MwanaFA)
Sielewi lugha nyingine/
Macho yamegoma hayaoni kiumbe mwingine/
Huyu ntakopa ntaazima/ila lazima/
Ninyooshe mji mzima/
Acha moyo unibebe unipeleke unapotaka/
Ntarudi siku ukitaka/
Im all in, Im fallin’/
Maskio yataniziba akiniita darling/
Moyo unanienda mbio,naisoma namba/
Mwili mlaini utasema aliumbwa kwa pamba/
Hana chale hana shanga/
Mimacho imentoka ile kishamba/
Sina hakika ni chiicha au ganja za zamani/
Ila ana siifa za kuitwa mwandani/
Tuchangie shuka,tuchangie majina/
Nimshike mkono niende nae dunia nzima/

HOOK

MAUA SAMA:
Umetokea wapi kwani?/
Na umetumwa na nani?/
Umekuja na uganga wa wapi?/
Nilikuwa sawa kabla sijakutia machoni/

Sielewi Sielewi Eeh,Eeh
Sielewi Sielewi Eeiiih,Eeeh

HOOK

Hata Sielewi naona nyota mamaa
Hata Sielewi naona nyota mamaa
Post a Comment
Powered by Blogger.