Diddy Awaongoza Beyonce Na Drake Kwenye Orodha Ya Wanamuziki Waliolipwa Pesa Nyingi 2017


Unamfahamu kwa jina la Puff Dady, P.Diddy au jina Diddy au  Brother LOVE, AKA yake aliyoitangaza juzikati alipokua akisherehekea Birthday yake ya 48. Jina lingine ambalo linaweza kumtambulisha rappa huyo kutokea Marekani ni kinara wa wanamuziki walioingiza mkwanja mrefu zaidi kwa mwaka 2017. Anatajwa kutengeneza zaidi ya dola 130 za kimarekani zilizotokana na ziara aliyoifanya baada ya kuungana na timu yake ya Bad Boy Family, deal ya Ciroc Vodka na mauzo ya 1/3 ya brand yake ya nguo (Sean John) pekee ambayo  yametajwa kufikia dola milioni 70.


Akijitengenezea mkwanja unaofikia dola milioni 105 Queen Bey (Beyonce) ametajwa kama mwanamuziki wa pili kuingia kwenye orodha ya wanamuziki waliojiingizia mkwanja mrefu zaidi, Ziara ya Albamu yake "Formation" iliyofanyika mwishoni mwaka jana (2016) imetajwa kama chanzo kikubwa cha mapato ya muimbaji huyo.

Baada ya kuwa Mwanamuziki ambae nyimbo zake zimekua zikisikilizwa zaidi kwa miaka kadhaa Drake ameangukia nafasi ya 3 miongoni mwa wanamuziki walioingiza mkwanja mrefu kwa kutengeneza dola milioni 94 asilimia kubwa zikiktokana na Boys Meets World Tour.

List Kamili Ya 10 Bora Hii Hapa:

1) Diddy ($130m)

2) Beyonce ($105m)

3) Drake ($94m)

4) The Weeknd ($92m)

5) Coldplay ($88m)

6) Guns N' Roses ($84m)

7) Justin Bieber ($83.5m)

8) Bruce Springsteen ($75m)

9) Adele ($69m)

10) Metallica ($66.5m)

Justin Bieber ameonekana kuwa mwanamuziki mdogo zaidi kuingia kwenye Orodha hiyo akiwaacha chini Adele,Bruce Sprinsteen na Metalica, Bieber ametajwa kuingiza dola milioni 83.5 huku vyanzo vikubwa vya mapato hayo vikitajwa kuwa zaidi ya Live Shows 100 alizopfanya mwaka huu, deal ya Calvin Klein, Emoji zake (JustMoji) na streaming za ngoma zake ikiwemo Despacito aliyoshrikishwa na Luis Fonsi. 


Orodha Ya FORBES Ya Wanamuziki Wa Hip Hop Wenye Umri Chini Ya Miaka 30 Waliofanya Makubwa 2017:


Post a Comment
Powered by Blogger.