@WizkidAyo - Ojuelegba (TBT MUSIC)Ojuelegba ni wimbo unaopatikana kwenye Aalbamu "Ayo" ya mwanamuzki Wizkid wa Nigeria.

Wimbo umeandikwa na Wizkid huku kwenye uaandaji kundi la Legendury Beatz ndio wamehusika kuikamilisha. Ojuelegba inaelezea shida na changamoto zote ambazo Wizkid alikutana nazo akiwa bado ni underground mpaka mafanikio aliyokua nayo kwa wakati huo.
Wimbo ulipata nafasi ya kusikikika karibu kwenye kila Radio Station zinazofanya poa Nigeria na nchi kadhaa za Afrika na kufanikiwa kushika namba 1 kwenye chati za Afrobeat ya Radio Capital Xtra.

Julai 2015 Remix ya “Ojuelegba” iliyowashirikisha Drake na muingereza Skepta ilisikika OVO Sound Radio ambayo pia ilifuatiwa na remix ya Mghana Sarkodie, Orodha ya ngoma 107 bora kwa mwaka 2015 ya Jarida la The Fader iliitaja ngoma hiyo kwenye nafasi ya 12.

Video ya ngoma hiyo iliyofanywa na Clarence Peters inamuonyesha Kondakta wa Daladala akiwaita abiria wanaoelekea mitaa ya Ojuelegba. Wizkid ni mmoja wa abiria wanaoonekana kudandia daladala hilo. Mfumo wa maisha kwenye mji wa Ojuelegba, vituko na mambo mengine mengi ambayo muimbaji huyo aliwahi kuyaishi akiwa hajulikani mpaka sasa anapozihesabu Baraka zake. Kwa ufupi video hiyo inaaongelea safari ya muziki wa Wizkid,Septemba 26,2014 Wizkid alipata nafasi ya kuperfom wimbo huo kwenye ukumbi wa Indigo At the 02 Arena Uingereza.


Post a Comment
Powered by Blogger.