Waziri wa fedha Wa Mugabe na Kiongozi wa ZANU-PF Mahakama yawanyima dhamana

Waziri wa zamani wa fedha wa Zimbabwe Ignatius Chombo na kiongozi wa tawi la vijana wa Zanu PF, Kudzai Chipanga waliofikishwa tena mahakama ya hakimu mkazi Harare jana, wamenyimwa dhamana.

Baada ya hatua hiyo mawakili wao walisema kwamba leo watakata rufaa Mahakama Kuu.

Wawili hao walikamatwa na kufikishwa kortini Jumamosi na walibaki mahabusu mwishoni mwa wiki wakisubiri dhamana yao Jumatatu lakini walinyimwa. Wanashtakiwa kwa masuala ya rushwa.

Mahakama hiyo iliambiwa kwamba wawili hao walitekwa na watu waliokuwa wamevaa sare za jeshi na wakabaki kizuizini kabla ya kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Ijumaa.

Inaaminika walizingirwa wakati jeshi lilipotwaa mamlaka ya nchi na kusababisha mzee Robert Mugabe aliyetawala kwa miaka 37 kujiuzulu.
Post a Comment
Powered by Blogger.