Nyoni Amuoneshea Ubabe Okwi

Beki wa klabu ya Simba, Erasto Nyoni amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba kutokana na kura zilizopigwa na wapenzi na mashabiki wa timu hiyo na kufanikiwa kumfunika mshambuliaji, Emmanuel Okwi ambaye ndiye anaeongoza kwa idadi ya magoli.




Nyoni amekabidhiwa tuzo hiyo na Meneja wa Simba SC Bw. Richard Robert hapo jana katika viwanja vya Polisi jijini Dar es Salaam ambapo kikosi cha Simba kilikuwa kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa jumapili hii dhidi ya Lipuli FC ya Iringa

Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyoa hufanywa kupitia Simba App, ambapo kila mwezi inautaratibu wa kutangaza mchezaji mmoja aliyefanya vizuri zaidi.
Post a Comment
Powered by Blogger.