Lukaku atengeneza history timu ya taifa Ubelgiji

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amekuwa mchezaji wa Ubelgiji ambaye ameweka rekodi ya ufungaji mabao mengi kwa timu ya taifa hilo.

Vijana hao wa Roberto Martinez waliifunga Japan bao 1-0 huko Brugge.
Lukaku , 24, alifunga goli la 31 kwa nchi yake pale alipomalizia krosi safi kutoka kwa Nacer Chadli aliyoiingiza wavuni kwa kutumia kichwa.

Lukaku alikuwa ametoshana na Bernard Voorhoof na Paul van Himst walipokuwa na magoli 30 kila mmoja wiki iliyopita.

Ubelgiji waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lukaku alifunga mabao yake ya kwanza ya kimataifa akichezea Ubelgiji nchini Urusi mwaka 2010
Mara yao ya mwisho kushindwa ilikuwa mikononi mwa Uhispania mechi ya kirafiki Septemba 2016.
Kwengineko, Uholanzi walipata ushindi wao wa pili tangu kukosa nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia nchini Urusi walipopokeza Romania kichapo cha magoli 3-0 huko Bucharest.
  • Mambo muhimu kuhusu nchi ambazo tayari zimefuzu Kombe la Dunia 2018
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel alifunga bao lake la kwanza la kimataifa tangu mwezi Mei 2008, pamoja na mchezaji mwenza Memphis Depay na Luuk de Jong.

Mabingwa wa Euro 2016 Ureno walitoka sare 1-1 na Marekani, wakicheza bila nyota wao Cristiano Ronaldo. Vitorino Antunes alikomboa bao lililokuwa limefungwa na Mmarekani Weston McKennie mapema mwenye mechi Leiria.
Post a Comment
Powered by Blogger.