G-eazy atangaza ujio wa albamu yake

Orodha ya mastaa wanaotarajia kuachia albamu zao mwaka huu, inazidi kuongezeka kwani mtu mzima G-eazy ametangaza kuachia albamu yake ‘The Beautiful & Damned’ ifikapo Desemba 15 mwaka huu.

Rapper huyo tayari alisha achia ngoma yake ‘No Limit’ mwezi Septemba mwaka huu, ambapo amlimshirikisha rapper wa kike anayesumbua kwa sasa Cardi B pamoja na rapper Asap Rockya.
G-eazy tayari ameshaachia kava ya albamu hiyo ila bado hajabainisha ni ngoma ngapi mpaka sasa zitapatikana katika albamu yake tano ya ‘The Beautiful & Damned’.

Mastaa kama Dj Khaled, Jay Z, Chris Brown, Willow Smith na wengineo wameachia albamu zao kwa mwaka huu ila pia bado kuna msafara wa albamu zizinge kutoka kwa mastaa kama Wiz Khalifa, Taylor Swift, Miguel na wengineo kuachia albamu zao kabla ya mwisho wa mwaka na huwenda idadi ikaongezeka pia.
Hizi ni baadhi ya albamu za G-eazy:
1. The Epidemic LP – Julai 10, 2009
2. Must Be Nice – Septemba 26, 2012
3. These Things Happe – Juni 23, 2014
4. When It’s Dark Out – Decemba 4, 2015
Post a Comment
Powered by Blogger.