#Forbes30Under30: Watoto 3 Wenye Umri Mdogo Zaidi Wenye Ushawishi

1: Marley Dias
Marley Diaz ni msichana wa miaka 12 amezaliwa Philadelphia Marekani, ni mwandishi wa Vitabu ambae alianza kupata maarufu baada ya kuzindua kampeni yake ya #1000BlackGirlBooks mwaka 2015.

Kupitia kazi yake ya Marley ameshapata mialiko sehemu zenye hadhi za juu ikiwemo Ikulu ya Marekani alipohudhuria na kupata nafasi ya kuongea kwenye mkutano wa Wanawake wa Marekani ambao pia ulihudhuriwa na Firstlady wa kipindi hicho Michelle Obama na Oprah Winfrey.


2: Henry Burner


Akiwa na umri wa Miaka 14 tayari Henry ameweza kuwa na kampuni yake "ButtonSmith" inayouza bidhaa kama vishikizo, Nembo, Vizuia Vitambulisho. Alianza kwa kuwauzia wanafunzi wenzake shule kabla ya kuhamia kwa watu wazima na mpaka sasa Henry ameajiri wafanyakazi 9 watu wazima.

Peyton Robertson:


 Peyton Robertson ni miongoni mwa wanasayansi wenye umri mdogo akiwa na miaka 17 tayari anazo medali tano za Ugunduzi wa vitu. Peyton ni mgunduzi wa Taasisi ya kujitolea ya kuwafundisha watoto mafunzo ya Sayansi, Teknolojia, Mahesabu na Uhandisi.

 

Orodha Ya FORBES Ya Wanamuziki Wa Hip Hop Wenye Umri Chini Ya Miaka 30 Wanaofanya Makubwa 2017:

Post a Comment
Powered by Blogger.