Askari Wa Korea Aliyepigwa Risasi Amepata Nafuu


Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ambaye alipigwa risasi 6 alipokuwa akivuka mpaka wa nchi hiyo, katika harakati za kutoroka, amepata afueni na sasa anaweza kuwasiliana na wahudumu wa kimatibabu.

Madaktari wanasema kuwa wamemtaka atizame runinga na kwa sasa anaonyeshwa filamu za Korea Kaskazini.
Wiki iliyopita, askari huyo aliamua kulitoroka taifa hilo, kwa ujasiri mkubwa, ili kuingia kwenye ardhi ya taifa jirani la Korea Kusini, hatua iliyowalazimu wanajeshi wenzake kummiminia zaidi ya risasi 40, huku sita zikimpata.

Wengi walidhani amefariki, lakini kwa kudra za mwenyezi Mungu, yungali hai.

 Wafanyakazi katika Hospitali hiyo wanasema kuwa japo askari huyo anahuzuni nyingi, wamemwekea bendera ya Korea Kaskazini ukutani karibu na kitanda chake, ili kumliwaza.


Moto Ulivyowaka CloudsFM MikocheniPost a Comment
Powered by Blogger.