Mwanamke Anaetarajiwa Kuwazalia Kanye West Na Kim Kardashian Anadaiwa Kuwa Sehemu Isiyojulikana

Taarifa za Rappa Kanye West na babymama wake Kim Kardashian kujiandaa kumpokea mtoto wao wa 3 atakaezaliwa mwezi Januari 2018 bado zinaendelea kuwa stori kubwa kwani kila kukicha mitandao blogs na TV hazikosi cha kusema.


Kama ilivyotangazwa awali kuwa wanandoa hao wanatarajia kupata mtoto huyo kwa njia ya upandikizaji kwa mwanamke waliyemlipa baada ya Kim Kardashian kugundulika kuwa na tatizo kwenye mfumo wake wa uzazi.

Kwa mujibu wa TMZ wakati Kanye na Kim wakiwa busy kuandaa mazingira watakayompokelea mtoto wao huyo mama mjamzito anadaiwa kutoonekana kwa muda sasa. "Mawasiliano yao sio hafifu wanawasiliana na amekua akitoa taarifa muhimu kuhusu hali ya ujauzito wake". Chanzo cha karibu na familia hiyo kimeiambia TMZ.
Post a Comment
Powered by Blogger.