Watumiaji Wa Twitter Sasa Kuandika Tarakimu 280Mtandao wa Twitter umetangaza kuanza kuwafungulia watu wanaoutumia mtandao huo uwezo wa kuandika kwa kutumia tarakimu 280 badala ya 140 zilizokua zikitumika kabla.
Kampuni hiyo ilikuwa imewawezesha baadhi ya watu kutumia tarakimu hizo lakini kwa majaribio tangu mwezi Septemba.
Twitter wamesema majaribio yalifanikiwa.
Mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango wa Twitter kuwavutia watu zaidi.

Lakini sasa wamesema watu wengi wataruhusiwa kuandika ujumbe mrefu.
Watakaozuiwa kutumia tarakimu 280 ni wale wanaoandika Kijapani, Kichina na Kikorea kwasababu wanaweza kuwasilisha maelezo zaidi kwa kutumia tarakimu chache.


Wakati wa majaribio, ni ujumbe 5% ambao ulikuwa na urefu wa zaidi ya tarakimu 140 na ni 2% uliokuwa na zaidi ya tarakimu 190,
Lakini walioandika ujumbe mrefu walipata wafuasi zaidi, walibadilishana mitazamo na na watu wengi zaidi na walitumia muda zaidi katika mtandao huo.


Mabadiliko hayo yalipotangazwa mara ya kwanza, wengi waliyakosoa na kusema badala yake wangependa kuona taarifa za chuki pamoja na mashine zinazoandika ujumbe zikidhibitiwa zaidi.

Mtandao huo kwa sasa una watumiaji milioni 330, idadi ambayo ni ya chini ukilinganisha na milioni 800 wa Instagram na zaidi ya  bilioni 2 wanaoutumia Facebook.
Powered by Blogger.