Raila Odinga Kukabiliana Na Rais Uhuru Kenyatta


Bwana Raira Odinga sasa yuko tayari kukabiliana na Rais Uhuru Kenyatta anaye waniya nafasi ya muhula wa pili kupitia chama cha Jubilee  katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka 2017.

Mgombea huyo Bwana Raira Odinga amesema "Hii ni heshma kubwa sana ambayo ndugu zangu wamenifanyia kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA," kwenye hotuba baada ya kuteuliwa na Muungano wa vyama vya upinzani nchini kenya National Super Alliance (NASA).Amesema Sisi tuko kama timu yenye pembe tano (Pentagon) wamenipa utepe wa nahodha,hiyo inaniunganisha mimi nao na Wakenya wote,tutatembea pamoja bega kwa bega.
Tunataka kubadilisha na kutekeleza ndoto ya Waanzilishi wa Taifa letu".

Alisema serikali yake itaangazia kumaliza umaskini,kuimalisha Afya,kuboresha uchumi,kubuni nafasi za kazi na kelejesha gharama ya Elimu na maisha chini.

Mgombea huyo pia ameahidi Walimu na Madaktari,pamoja na wafanyakazi wengine wanalipwa mishahara vizuri kadhalika ameahidi kuthibiti rushwa nchini humo.

 Aliendelea kwa kusema kuwa atakuwa kama nabii Joshua kwenye Bibilia na kuwavusha wakenya hadi nchi ya ahadi.Powered by Blogger.