Hizi Hapa Aina Za Simu Ambazo Hazitambuliki Na WhatsApp
Huduma ya WhatsApp haitumiki tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.
Hii inakuja baada ya kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo kusema inataka kuboresha zaidi huduma katika huduma hiyo inayotumiwa na watu wengi.
 Mabadiliko hayo ya WhatsApp, yalipangiwa kuanza kufanya kazi katika tangu mwishoni mwa Desemba 2016. Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka jana.


Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.
Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.


Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:

  • Android 2.1 na Android 2.2
  • Windows Phone 7
  • iPhone 3GS/iOS 6


Simu ambazo wateja wake hawataweza kutumia Whatsapp ifikapo Juni 30, 2017 ni:
  • BlackBerry OS and BlackBerry 10
  • Nokia S40
  • Nokia Symbian S60
Wanaotumia simu za aina hiyo wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.
Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.

Powered by Blogger.