Big Sean Sio Wa MchezoMchezo Cheki Alichokifanya Instagram Baada Ya Kukutana Na Post Ya Jhene


Kama ni mfuatiliaji wa mastori kuhusiana na maisha ya mastaa wakubwa hii ya mapenzi kati ya Big Sean na Jhene Aiko inakua sio inshu ngeni kwako, Jamaa ni moja kati ya zile couple zinazokiki kinoma kwenye ulimwengu wa burudani, kufuatia upendo unaoonekana machoni mwao ni wazi Big Sean na Babymama wake Jhene waliumbwa kulikamilisha hilo.

Hivi juzikati mrembo Jhene akiwa pande za LA kwenye utoaji wa Tuzo za FLAS alitupia picha kwenye ukurasa wake wa instagram na kuisindikiza na caption ambayo ilimuonyesha kabisa kuwa naye sio mtu wa mchezomchezo "Caption hiyo yenye maneno magumu kidogo kwa watoto chini ya miaka 18 ilisomeka "

"Jinsi ninavyomuangalia akishamaliza safari zake za kikazi, namfungia chumbani kwangu na ninahakikisha mlango umefungwa ndani ya masaa 72" aliandika Jhene, Sasa masaa kadhaa badae mnyamwezi Sean si akaisanukia post hiyo unajua alisemaje?, Cheki pichani hapa chini

 "Man the countdown is real" ndio majibu ya Big Sean kwa mujibu wa komenti aliyoiacha kwenye picha hiyo.


Powered by Blogger.