YANGA YALIPIZA GOLI MBILI KWA RUVU SHOOTING


Klabu ya Yanga kutoka Jangwani imegawa dozi kali leo kwa Ruvu shooting ni baada ya kuwa na mzigo mzito wa goli mbili walizopewa na Watani wao jadi wa Msimbazi klabu ya Simba imetua mzigo wa goli hizo.

Wakimataifa hao wamezirudisha goli hizo mbili kwa Klabu ya Ruvu shooting kutoka Pwani kwa kuwafunga goli mbili kwa bila goli la kwanza likifungwa na mshambuliaji wake Simon Msuva dakika ya 31 na sekunde 22 kwa njia ya Penati na goli la pili likifungwa na mchezaji wao waliomsajili dirisha dogo Emmanuel Martin kwenye dakika ya 94 kwakupiga kichwa kikali kilichokwamishwa na nyavu za Ruvu shooting  kwa kupokea mpira uliopigwa na yuleyule mfungaji wa goli la kwanza Simon Msuva na kwa upande mwingine wa Klabu ya Yanga walizawadiwa kadi nyekundu kwenda kwa mshambuliaji wake kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa.
Powered by Blogger.