YANGA KUKIPIGA LEO NA RUVU SHOOTING TAIFA


Klabu ya Yanga leo wanakibarua kingine leo dhidi ya Ruvu shooting katika Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Hiyo ni baada ya juzi tu Jumamosi kutoka kwenye kipigo kikali cha goli 2-1 kwenye ule mtanange dhidi ya wahasimu wao yani Mnyama Simba.Ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza michezo 22 kikosi hicho cha kocha Mzambia, George Lwandamina kitalazimika kushinda mchezo wa leo ili kupunguza ‘gepu’ la pointi tano dhidi ya vinara Simba ambao tayari wamecheza michezo 23.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Tanzania inakutana na Klabu hiyo kutoka Pwani Ruvu Shooting katika muendelezo wa ligi kuu nchini ikiwa pia inakosa huduma ya wachezaji wake watatu wa kigeni ambao ni Donald Ngoma na Thabani Kamusoko kutoka nchini Zimbabwe kwa kuwa na majeruhi na beki wake raia wa Togo Vincent Bossou kwa madai ya kudai mshahara wake.

Powered by Blogger.