Wema Sepetu Amuunga Mkono Paul Makonda Juu Ya Jambo Hili


Miss Tanzania 2006 Mrembo Wema Sepetu ambae ni Kamanda mpya wa Chama cha CHADEMA ameadhimisha siku ya Wanawake kwa kupanda miti huko mkoani Morogoro na katika kile kinachoonekana ni kulinda mazingira.

Wema Sepetu ametumia mawazo yale yale ya kampeni ya ‘Mti wangu’ ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda ambayo ilikuwa na lengo la kulinda mazingira.


So huenda Wema Sepetu akatumia ushawishi wake kutangaza kampeni kubwa za kulinda mazingira kwani kwa sasa nchi yetu imekumbwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kwa hilo kila mtanzania atamsapoti Wema Sepetu namshauri pia kampeni hiyo ianzie mkoani Dodoma ambako hali ya ukame imekithiri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika... "Leo ni siku ya wanawake Duniani, na kama mwanamke nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabili ya Maji… Wote tunajua kuwa mwanamke ndo anaekerwa zaidi katika upatikanaji wa maji… Labda haitotusaidia leo wala kesho, lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu hapo baadae…. Morogoro ni eneo linalosadikika kuwa Chanzo cha Maji hata yale tunayotumia Mkoani kwetu (Daressalaam)… Ninajiskia faraja kuwa kutakuwa na helping hand yangu somewhere when it comes to Water supply in my society… Mazingira yetu hayana Itikadi wala Vyama, Yanagusa kila mtu… I feel honored to be part of this activity… Tumetoka Kata ya Kilakala and now tunaelekea kwenye Chanzo kingine kinachoitwa Mambogo.
Powered by Blogger.