WAZIRI NAPE NNAUYE AUNDA KAMATI KWA AJILI YA SERENGETI BOYS

Waziri mwenye dhamana ya Sanaa na Utamaduni,Michezo nchini Tanzania Nape Moses Nnauye ameteua kamati ya uhamasishaji.

Kamati hiyo ni kwa ajili ya Timu ya Taifa wa umri chini miaka 17 vijana wa Serengeti boys wanaoelekea nchini Gabon katika mashindano ya AFCON 2017.
Kamati hiyo aliyoitaja waziri inawahusisha watu kumi ikiongozwa na Mtangazaji Charles Hilaly kutoka Azam tv akiwa ni mwenyekiti akifatiwa na Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba na Mtangazaji wa E-fm redio Maulid Kitenge na pia mwanadada aliyekuwa miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu na wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva Diamond na Ali kiba nao wakiwemo kwenye kamati hiyo.


Powered by Blogger.