Orodha Ya Wanamuziki Ambao Wameanza Kuuza Muziki Wao Kupitia Wasafidotcom

Wasafi.com imeendelea kukusanya idadi ya wasanii wa muziki amabao wamekua tayari kuuza muziki wao kupitia tovuti hiyo pendwa, Mpaka sasa wasafidotcom imefanikiwa kuwa na jumla ya wasanii 21 ambao muziki wao unapatikana kwenye tovuti hiyo.

1:Ray C:

Unaweza ukawa haujamsikia kwa muda mrefu kwenye masikio ya ulimwengu wa muziki lakini kaa ukijua mwanadada Ray C hajaupiga chini muziki, Kitu ambacho unatakiwa kujua Ray C ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kabisa kujiunga na wasafidotcom.

2: Dulla Makabila:
 Haina ubishi kama jamaa ndie mbabe wa singeli kwa sasa kutokana na mapokeo mazuri ya ngoma zake"Tabia Yake" na "Ujaulamba" ambayo ndio habari ya mjini kwa sasa, Hizo zote unazipata sehemu moja kwenye tovuti ya wasafidotcom.

3:Tanayzer:


 Uliisikia sauti ya huyu mshikaji kwenye mdundo wa Producer LizerClassic?, Ofcoz ni ile Guta ngoma ambayo imemkaribisha vizuri kwenye game ya bongoflava nayo ni miongoni mwa ngoma zinazouzwa na wasidotcom.

4; Billnass 
 
 Mwenyewe anajiita Mzungu Mzee, Bilnass nae ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kabisa kujiunga na platform hii ya uuzaji muziki ya wasafidotcom, Chafu Pozi, Ligi Ndogo na Mazoea zote unazipata wasafi.com

5: Barnaba;
 Barnaba ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajawahi kushuka kimuziki tangu alipotoka kwa mara ya kwanza mwaka 2005, wasafidotcom imethibitisha kuuza muziki wake.

6: Professor J 

 The Heavy Weight MC moja kati ya waasisi wa muziki wa bongo, kupitia wasafi.com juzikati alitambulisha ngoma yake "Kibabe"  ya kwanza kwa mwaka huu 2017

7; Belle9
Kutoka "Sumu Ya Penzi" mpaka "Give It To Me" na ngoma zake zote zenye vitamini Belle9 amethibitisha kuuza muziki wake kupitia wasafi.com

8: Navvykenzo
Kuna tatizo kwani?, Wasafidotcom haiuzi single peke yake, Goodnews ni kwamba Albamu nzima "AIM" ya Navykenzo inapatikana wasafidotcom

9: Mrisho Mpoto
 Mjomba wako Mrisho Mpoto ameingia kwenye list ya wasanii wa kwanza kabisa kuwaunga mkono WCB kwa kukubali kuingiza muziki wake kwenye tovuti ya wasidotcom.

10: Kassim Mganga


Kassim Mganga kwenye ngoma yake mpya "Somo" amewapa Shavu "The Kilimanjaro Band" ngoma imeendelea kufanya poa mitandaoni kwenye radio na TV.. Ukiachana na hiyo ngoma zote za Cassim Mganga unazipata wasafi.com

11: Chege Na Temba 

 Siku chache zilizopita wakataa mkaa wa Temeke Chege Chigunda na Mh Temba waliutambulisha mzigo wao "Go Down" kwenye radio mbalimbali na hatimaye kuufikisha wasafi.com
 
12: Timu Nzima Ya WCB:

 Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Harmonize na Big Boss wa WCB yaani "Diamond Platnumz wanaikamilisha list hii kwa kutengeneza idadi ya profile za wanamuziki kufiki 21 kwenye tovuti hiyo.
 

 

Powered by Blogger.