Universal Music yaipiga pini ShEther ya Remy Ma, ni kwa kutumia beat ya Nas na kuuza wimbo bila ridhaa yaoDiss track ya Remy Ma kwa Nicki Minaj, ShEther haipigwi tena kwenye redio nyingi za Marekani na pia imetolewa kwenye mtandao wa Soundcloud.

Hatua hiyo imechukuliwa na kampuni ya Universal Music Publishing, inayoilimiki beat hiyo iliyokuwa wimbo wa Nas, Ether.

Universal imemind baada ya Remy kuanza kujipatia fedha kupitia wimbo huo wakati hakupewa ruhusa. Vyanzo vilivyo karibu na Remy, vimeiambia TMZ kuwa amekatazwa hata kuutumbuiza wimbo huo.

Universal waliamua kuwa wakali baada ya “shETHER” kushika namba No. 2 kwenye iTunes. Kwa upande wake, Nas inasemekana hata tatizo na beat yake kutumika na kwamba ni shabiki wa vita katika rap.
Powered by Blogger.