SIMBA YATUA ARUSHA KUWAKABILI KLABU YA MADINI HUKU BLAGNON AKIJIUNGA NAO


Klabu ya Simba inaendelea na maandalizi ya mazoezi ilikuwakabili klabu ya Madini FC katika michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya robo fainali mechi itakayopigwa Jumapili hii katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid - Arusha.

Huku mchezaji wake wakimataifa kutoka Ivory Coast Fredrick Blagnon aliyetolewa kwa mkopo Uarabuni nchini Oman katika klabu ya Fanja akiwa amejiunga nao baada ya msemaji wa klabu hiyo ya Simba akinukuu kuwa amerejea kwa sababu ya kutokikizi vibari vya ITC.

Wekundu hao wameanza mazoezi leo ya kujiweka sawa katika viwanja vya TGT mkoani Arusha, mara ya baada ya kumaliza ziara yao mkoani Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange “Kaburu” amesema: “Kwa kuona umuhimu wa mchezo huo, tumehamua kuwahi mapema ili kuzoea hali ya hewa ya mkoa hapa (Arusha).” “Tunachukulia kambi hii kama sehemu ya maandalizi ya mechi zetu tatu za Kanda ya Ziwa ambazo tunaamini kwa kikosi chetu tutaondoka na pointi zote tisa.
Simba wanakabiliwa na mechi ngumu za Kanda ya Ziwa ambako watakuwa na mechi tatu za ligi kuu dhidi ya Toto Africans, Mbao FC zote za jijini Mwanza na Kagera Sugar ya Bukoba mkoani Kagera.


Powered by Blogger.