Shilole Akanusha Madai Ya Kuwa Mjamzito


Msanii filamu na muziki wa bongo fleva, Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana ujauzito wowote bali ameridhika na maisha jambo ambalo limefanya aongezeke mwili na kunenepa licha ya watu kuwa na hisia kuwa huenda ana ujauzito.

"Mimi saizi sina ujauzito wowote sema nimenenepa tu maana nimeridhika na maisha haya haya, ukimya wangu ni kwa sababu nilikuwa nazipa ngoma nafasi saizi nimeamua kuja rasmi na wimbo wangu huu 'sitoi kiki' kwani nimegundua Watanzania wanataka burudani, saizi pesa hakuna hivyo nimeona bora nije kuwaliwaza na muziki mzuri huu" alisema Shilole kwenye kipindi cha 5SELEKT.
Powered by Blogger.