Samir Nasri amchana Guardiola adai ni kigeugeu aliyekataa kumsikiliza kuhusu kubaki Man City


Kumbe Samir Nassri aliambiwa na kocha wake, Pep Guardiola hasiondoke lakini straika huyo aliamua kusepa! Alipoulizwa kwanini aliamua kuondoka, Samir alijibu: 

“Kocha Pep ni mtu kigeugeu na haaminiki, hivyo isingekuwa rahisi kwangu kumkubalia kubaki maana nisingekuwa na namba ya kudumu.”

“Niliamua hilo kwa maslahi ya kiwango changu cha soka kwasababu nilikuwa nahitaji kuendelea kucheza katika kikosi cha kwanza.”

Kauli hii ya Nasri inakuja wakati huu ambapo anakaribia kutiomiza mwaka mmoja ndani ya kikosi cha timu yake ya sasa ya Sevilla inayoshiriki La Liga nchini Hispania.

Katika mazingira yasiyo ya kawaida, Nasri alimeza mate ya akili na kumkatalia kocha wake huyo kwa kile alichodai kuwa uwezekano wa namba katika kikosi cha Manchester City ni mdogo.

Nasri aliingia katika kapu la wachezaji ambao tangu kocha Guardiola atue Manchester City wamekuwa hawana nafasi katika kikosi cha kwanza.

Wachezaji hao ni pamoja na Joe Hart, Wilfried Bony, Eliaquim Mangala na Jason Denayer ambao ni kama walionyeshwa mlango wa kutokea mapema.

Nasri mwenye umri wa miaka 30, alisema: “Guardiola alitaka nibaki City kwa ahadi ya kuwa nitapata namba kikosini.”

“Lakini nilimkatalia nikitambua kuwa kauli yake haikuwa na ukweli halisi. Mimi ni mchezaji na ninahitaji kucheza siku zote ili kulinda kiwango change kisishuke.”

“Nimejiunga Sevilla ikiwa ni timu ambayo ni kama familia yangu. Nina uhakika wa kucheza nikiwa hapa.”
Powered by Blogger.