Sakata la Madawa: Vanessa Mdee Akamatwa na Polisi, Yadaiwa Apelekwa kwa Mkemia Mkuu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Akizunguzumzia taarifa hiyo, Mwanasheria wa mwanamuziki huyo, Amin
Tenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Vanessa
alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi kama alivyoagizwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitaja majina ya watuhumiwa wa
dawa hizo mapema mwezi uliopita.
Vanessa ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa
wa dawa za kulevya, lakini hakuweza kuripoti kwa wakati sababu alikuwa
nchini Afrika Kusini kikazi.
Baada ya kujisalimisha, Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi nyumbani
kwake kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wwa Serikali kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
Jeshi la Polisi hadi sasa halijatoa taarifa kuhusu tukio hilo na kama walikuta ushahidi wowote nyumbani kwa mwanamuziki huyo.