RIDIHIWANI: NILIITWA KUHOJIWA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

 
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa aliitwa na kamishna wa tume ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini na kuhojiwa juu ya sakata la madawa ya kulevya.

Ridhiwani amekiambia kipindi cha Habari Extra kuwa mahojiano hayo yaliisha kwa yeye kuachiwa kwa kuwa walibaini kuwa hausiki hata kidogo na matumizi au uuzaji wa madawa ya kulevya.

“Ukweli ni kwamba niliitwa kwakua jina langu lilitajwa kwenye orodha ya watuhumiwa na nilionana na timu yake nzima walinihoji juu ya sakata hilo lakini hawajabaini jambo lolote linalonihusu kwenye madawa ya kulevya hivyo waliniachia huru ila walinipa angalizo kuwa niepuke kukaa kwenye baadhi ya maeneo.”
Powered by Blogger.