REAL MADRID WAKIZIDI KUJIKITA KILELENI BARCELONA WAKIWA CHALII


Wababe wa Santiago Bernabeu wamezidi kujikita kileleni baada ya jana kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Betis nyumbani kwao.
Wageni Real Betis ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya Antonio Sanabria kufunga akitumia vyema makosa ya kipa wa Real Madrid,Keylor Navas na kutumbukiza mpira kimiani.Navas nusuru aonyeshwe kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Darko Brasanac.

Cristiano Ronaldo aliifungia bao la kusawazisha Real Madrid akiunganisha vyema krosi ya Marcelo na kuandika bao lake la 26 la msimu kabla ya Sergio Ramos kufunga bao la ushindi.

Ushindi huo umeipeleka Real Madrid kileleni mwa msimamo wa ligi ya La Liga baada ya kufikisha pointi 62.Pointi mbili mbele ya Barcelona yenye pointu 60.Ikumbukwe Real Madrid ina mchezo mmoja pungufu.
Kwa wapinzani wao klabu ya Barcelona wao walipokea kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa klabu ya Deportivo la Coruna katika dimba la Estadio Municipal de Riazor wakiwa Ugenini.

Powered by Blogger.