Rais Magufuli: “Nawapenda Sana hawa SHILAWADU…”

Unaweza ukadhani kuwa Rais wetu huwa hafuatilii na wala hanaga muda na haya mambo ya SHILAWADU, lakini kumbe ni shabiki mkubwa wa kipindi hicho kinachoendeshwa na Mtangazaji wa Clouds FM Radio Soudy Brown pamoja na co-host wake Kwissa.

Akizungumza LIVE kupitia kipindi cha asubuhi cha Clouds TV, Clouds 360 ambapo msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz alikuwa mgeni mualikwa kwa siku ya leo, Rais Magufuli alikiri kutambua juhudi za wasanii wa Bongo Fleva kwenye kuitangaza nchi kupitia muziki pamoja na kukiri kuwa yeye ni mpenzi mkubwa wa SHILAWADU.
 
“Asante sana nimekusikia, na pia nakupongeza sana kwa kuzidi kuitangaza Tanzania katika masuala ya Muziki na nawapongeza wanamuziki wote, hata wale wanaoigiza nawapenda sana wale… SHILAWADU n.k, nawapenda sana. “- Alisema Rais Magufuli.
Powered by Blogger.