RAFU MBAYA ILIYOMPELEKEA FERNANDO TORRES KUTOLEWA UWANJANI NA AMBULANCE

Mchezaji wa klabu ya Atletico de Madrid ya nchini Hispania Fernando Torres usiku wa jana alipata itilafu ya ghafla uwanjani na kupelekea kushtua watu.

Mchezaji huyo raia wa nchini Hispania aliyezichezea vilabu kama Chelsea na Liverpool kwa sasa anaichezea klabu ya Atletico de Madrid usiku wa jana  alishtua mashabiki wa soka na wachezaji wenzake kwa ujumla kufuatia kupoteza fahamu nakupelekea kutolewa nje na gari la wagonjwa (Ambulance) na kufanya kila mchezaji aliyepo uwanjani kushtuka na watu wa soka kwa ujumla.
  kupoteza fahamu huko ni baada ya kuchezewa rafu mbaya ya kusumwa na kujigonga chini na mchezaji wa upinzani Alex Bergantinos kwenye dakika ya  85.
Hiyo ilitokea katika mchezo wa ligi kuu ya nchini humo ilipozikutanisha klabu ya Atletico de Madrid dhidi ya Deportivo la Coruna na mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 1-1.


Powered by Blogger.