Nay wa Mitego afunguka juu ya suala zima la Uchungaji


Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa, kwa sasa anawaza jinsi ya kujenga kanisa ili watu wamwabudu Mungu lakini hana ndoto za uchungaji kwa sababu haijui Biblia vizuri.
 
Nay alisema kuwa, baada ya kutangaza kujenga kanisa ambalo watu hawatatoa sadaka litakuwa kwa ajili ya kumwabudu Mungu, watumishi wengi wa Mungu walishtushwa na kauli yake hivyo anawatoa wasiwasi kwamba hana mpango wa kuwa mchungaji.

Alisema kuwa, yeye atajenga kanisa maeneo ya Mbezi Mwisho, Dar na watakuwepo wachungaji kwa ajili ya kuwafundisha watu Neno la Mungu na siyo yeye kama yeye.

“Sina ndoto za kuwa mchungaji maana sijui hata Neno la Mungu vizuri, nimeguswa kujenga kanisa tu ili watu wamwabudu Mungu kwa kuwa amenijalia kipato hivyo nafanya kama kutoa shukurani kwake. Kanisa hilo halitakuwa kwa ajili ya sadaka bali kumwabudu Mungu,” alisema Nay kwenye mahojiano na Risasi Vibes .
Powered by Blogger.