Nape Aunda Kamati Vita Ya Clouds Media Na Mkuu Wa Mkoa Paul Makonda

 
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nauye ameunda kamati maalumu itakayofanya kazi kwa siku moja kuchunguza kitendo kilichotokea cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuvamia Chombo cha habari Clouds Media siku ya ijumaa usiku.
 
Mhe Waziri amelaani kitendo hicho,na kuwataka waandishi wa habari kuwa watulivu katika kipindi hichi, wakati kamati hiyo inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Powered by Blogger.