Msanii Wa Hip Hop Bongo (JCB) Asema Anamkubali Darasa Wa Zamani Kuliko Wa SasaMsanii wa hip hop nchini Tanzania JACOB MAKALLA alimaarufu JCB  ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Arusha, Alisikika ktk kipindi cha LADHA3600 cha E.FM ambacho kinatangazwa na mtangazaji JABIR SALEH kuwa anampenda Darasa wa zamani kwakuwa ngoma zake zilikuwa kali alikuwa anazipenda piaa.

Hapo hapo akasema kuwa huyu Darasa wa sasa anampa RESPECT kwa kuirudisha Hip hop/Bongoflava ktk mstari au ktk ramani kutokana na wimbo wake wa MZIKI. Akaongezea kwa kusema kuwa mziki wa SINGELI kuna kipindi ulishaanza kuchukua nafasi mpaka kufikia hatua wasanii wakubwa wa Hip Hop nao kuimba singeli, Lakini hakuishia hapo akathubutu kusema kuwa hata radio kubwa nazo zilishaaanza kuusapoti mziki wa singeli na kutaka kuua mziki wa hip hop.

Mwisho akamalizia na kusema kuwa yeye kupiga picha na WCB ni kawaida kwani wale ni watu kama watu wengine, Na watu wengi wanao ongea ongea ovyo ktk mitandao ya kijamii wengi wao hawana family.


Powered by Blogger.