MICHAEL ESSIEN APATA TIMU YA KUICHEZEA


Staa wa zamani wa  chelsea ya England na Real madrid ya Hispania Michael Essien raia wa nchini Ghana leo March 14 2017 ametangaza kujiunga rasmi na timu ya Persib Bandung ya Indonesia.

Michael Essien alikuwa hana timu kwa kipindi cha miezi sita baada ya kuachana  na Panathinaikos ya Ugiriki mwaka 2016 na amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha akiba cha Chelsea kabla ya kujiunga na Persib Bandung.
Michael Essien mwenye umri wa miaka 34 alikataa kujiunga  na Merbourne ya Australia mwezi December mwaka jana.
Powered by Blogger.