MCHEZAJI WA LIVERPOOL ATUA NCHINI TANZANIA


Aliyekua mchezaji nguli wa klabu ya Liverpool John Barnes raia wa Jamaika atua nchini  Tanzania.

Mkongwe huyo wa klabu ya Liverpool John Barnes alitua nchini jana na kupokelewa na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said ,Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas.
Ujio wake ni kwa ajili ya mambo mbalimbali ikiwamo kusheherekea miaka mia moja ya Benki ya Standard Chartered ambao ni wadhamini wakuu wa klabu ya Liverpool na kuipa ujuzi timu ya Taifa ya Vijana  wa Tanzania "Serengeti  Boys" umri wa miaka 15 ambayo inatarajia kuwa wenyeji katika michuano ya mwaka 2019.
Pia kuwepo kwenye Bonanza ambalo Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda nchini Liverpool Uingereza.Timu zilizoingia fainali za mashindano hayo ya kikanda ni Azania Group ya Tanzania, Capital FM ya Kenya na Cocacola ya Uganda.
Nguli huyo hii inakua ni mara ya tatu kuja nchini Tanzania kwa shughuli mbalimbali za kijamii. 
Powered by Blogger.