MANCHESTER UNITED YAKWAMISHWA NA CHELSEA USIKU WA JANA


Usiku wa jana klabu ya Manchester United kutoka jijini Manchester wamekwamishwa darajani Stamford bridge na klabu ya Chelsea ya jijini London.

Usiku wa jana nchini Uingereza kulikua na mchezo wa FA cup uliozikutanisha vilabu vikubwa nchini humo klabu ya chelsea na klabu ya Manchester United iliyokuwa ugenini  waliobanwa mbavu na mahasimu wao wakubwa kutoka jijini London wenyeji klabu ya Chelsea baada ya kufungwa goli 1-0 likifungwa na kiungo wa chelsea Ngolo Kante nakutupwa nje kwenye kombe hilo la FA cup.
Hii inakua mara ya pili kwa mchezaji huyo kuifunga klabu hiyo tangu asajiliwe na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu huku goli lake la kwanza alifunga katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza

Chelsea ilipata ushindi huo dhidi ya Manchester United ambayo kwa takribani dakika 55 ilikuwa ikicheza pungufu baada ya mchezaji wake Ander Herrera kuzawadiwa  kadi nyekundu dakika ya 35 kwa kumchezea vibaya Edern Hazard.

Kwa sasa Chelsea watapambana na Tottenham Hospurs katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo huku Arsenal watapambana na Manchester City.


Powered by Blogger.