MANCHESTER UNITED KUKABIRIANA NA CHELSEA HII LEO


Klabu ya jijini Manchester Manchester United imefika jijini London kwa usafiri wa treni kuwakabiri wapinzani wao wenyeji klabu ya Chelsea ya jijini London.

klabu hizo zinamtanange usiku wa leo katika kombe la FA hatua ya robo fainali katika dimba la Stamford Bridge ikitarajiwa kuwa mchezo mgumu na mkubwa nchini Uingereza kwa kuwakutanisha makocha wawili wenye kupenda kutumia soka la kujihami na kushambulia.
Na wote ni makocha wenye vituko na mizuka wakiwa uwanjani na nje ya uwanja.
Katika mchezo huo, Man United itawakosa wachezaji wake Zlatan Ibrahimovic mwenye adhabu ya kufungiwa mechi tatu, Marcus Rashford na Anthony Martial pamoaja na nahodha wao Wayne Rooney ambaye aliaumia mazoezini.

Powered by Blogger.