MALAWI WAJITOA KUSHIRIKI CHAN NA AFCON HUKU ZAMBIA WAKITWAA KOMBE LA AFCON NYUMBANI


Shirikisho la soka nchini Malawi (FAM) limetangaza hivi leo kuwa timu yao ya Taifa ya Malawi haitashiriki mashindano ya CHAN na AFCON.

Shirikisho hilo limetangaza hivyo kutokushiriki kinyang'anyiro cha kufuzu kushiriki mashindano hayo makubwa barani Afrika ya CHAN mwaka 2018 yatakayo fanyika nchini Kenya na AFCON mwaka 2019 nchini Cameroun kwa sababu ya kuwa na ukata wa fedha na kutokupewa ushirikiano na Serikali ya nchi hiyo. wakisema kuwa Serkali yao ilikataa kutoa nusu ya fedha na wao Shirikisho kutoa nusu kwa ajili ya kumuajiri kocha kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho na ndipo kuamua kujitoa kushiriki katika kinyang'anyiro cha mashindano hayo kwa hatua ya kufuzu na huenda wakalazimika kutozwa faini na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF.
Suala hilo linawapa funzo baadhi ya Timu mbalimbali za Taifa zinazopata udhamini na kutokuzitumia vizuri kwa kufanya vibaya katika michezo yao.

 Kwa upande wa nchini Zambia wao wanafuraha ya kutosha kwa vijana wao wa umri wa miaka 20 kwanyakua kombe la AFCON kwa kuwatandika Vijana wa Senegal kwa goli mbili kwa bila mchezo huo ukishuudia na Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu na pia kuwakabidhi vijana wake kombe hilo na Rais wa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika Issa Hayatou.
Powered by Blogger.