Makonda Awatolea uvivu Wanaomtuhumu Mkewe


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewajibu wote wanaosema katika mitandao ya kijamii, kuwa mkewe si raia halali wa Tanzania na kusema kuwa, hata kila siku wataamka na kisa kipya yeye bado ataendelea kupambana na kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi.

Makonda ameyasema hayo alipokuwa ibadani katika kanisa la kiinjili la kilutheli KKKT Ushirikia wa Kimara ambapo alisema baada ya kuona wameshindwa kwa tuhuma hizi sasa wanaibua tuhuma zingine.

Aidha Makonda alisema kuwa anamfahamu historia ya vita dhidi ya madawa ya kulevya ya kuwa hakuna mtu aliyetoka salama. Wote walioanzisha mapambano haya hawakutona salama, wengi waliuwawa, wengine walifungwa na wengine walipata matatizo mbalimbali sababu wahusika wa biashara hii ni watu wenye nguvu.

Powered by Blogger.