MAKONDA AIKUMBUKA SEKTA YA MICHEZO KWA KUKARABATI VIWANJA VYA MPIRA

Serikali ya mkoa wa Dar Es Salaam chini ya Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda mwaka jana waliahidi kurekebisha baadhi ya viwanja vya mpira ambavyo vilivyokuwa vikitumiwa na Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup kwa kushirikia na Ubalozi wa China.

Mkuu wa mkoa huyo kwa jana alitembelea kiwanja kimoja wapo cha Boko Veteran ikiwa ni moja ya kujionea namna ya uboreshaji wake.

 Alisema hivi nukuu “Hapa tumefika ikiwa ni sehemu ya kuangalia shauku yetu kubwa ni kuona namna gani tunaweza kupata uwanja mzuri kwa sababu tuna vitu viwili, tuwe na uwanja wa nyasi bandia au uwanja wa nyasi halisi za kupandwa,” amesema Makonda alipotembelea uwanja wa Boko Veteran.
“Kwahiyo tumekuja hapa kuona sehemu ambayo ni maeneo yaliyotengenezwa kwa nyasi halisi, lakini uwanja tunaotarajia kuanza nao ni ule wa Bandari kwa sababu unatumika mara nyingi na wananchi wanaokaa maeneo ya jirani na pale.”
“Tunashirikiana na wenzetu wa ubalozi wa China ambao tulimuomba balozi wa China ambaye hayupo hapa lakini tumekuja na wasaidizi wake kwa ajili ya kuona lakini ndani ya wiki hii tutakuwa tumefanya maamuzi kama tutajenga uwanja wa nyasi bandia au nyasi halisi ili msimu wa Ndondo Cup utakapoanza angalau uwanja mmoja uwe umeshakamilika.”
Powered by Blogger.