Kweupee!! Muimbaji wa Kenya Susumila akubali kwamba yeye ni mchawi
Hatimaye msanii wa muziki kutoka Kenya Susumila amekubali kwamba anafanya uchawi ila ni wa aina yake. Kwa muda sasa, msanii huyu amekuwa akihusishwa sana na masuala ya ushirikina, hususan na wenzake wa kutoka Pwani ya Kenya ambapo ilisemekana kwamba anatumia nguvu za giza kuwazima wasanii wenzake kimuziki wakati akiendelea yeye.

Ijumaa ya tarehe 17 March, Susumila amejikuta akijibu swali hili kwenye kipindi cha Mambo Mseto kinachoruka kupitia Citizen Radio. Mtangazaji wa kipindi hicho Mzazi Willy Tuva alimuuliza iwapo yeye ni mchawi na sababu ya yeye kujiita ‘Wachawi International’.

Hakuona noma na moja kwa moja akajibu…”Eeh ni mchawi kwenye kufanya kazi”. Akaendelea, “Unajua ni mtu ambaye anafanya vitu ambavyo wengine wanafikiri havifanyiki. So mimi naweza kusema mimi ni mchawi kwa sababu nafanya vitu ambavyo wengine wanafikiri havifanyiki. Kukaa kwa muda mrefu, kufanya kazi ile ukitoa wanakubali.”

Kuhusu ishu ya kujiita Wachawi International, msanii huyo alidai kwamba jina lenyewe ni movement aliyoanzisha na mashabiki zake wanaielewa vizuri. Kwa sasa, Susumila anafanya vizuri na wimbo wake mpya kwa jina ‘Oyoo’. Ndani amemshirikisha msanii Timmy Tdat.
Powered by Blogger.