KUMBE PSG WALIENDA KUJIRUSHA KLABU NA RIHANNA KABLA YA KIPIGO CHA BARCELONA


Wachezaji wa klabu ya Paris St Germain kumbe kabla ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa klabu ya Barcelona siku mbili kabla walienda kumbi ya sterehe ya usiku.

Wachezaji hao wawili nafasi ya kiungo wanaoichezea klabu PSG ya nchini Ufaransa Marco Verrati raia wa Italia na Blaise Matuidi raia wa Ufaransa walienda katika kumbi ya starehe ya usiku jijini Paris wakiwa ni siku mbili mbele tu wanamtanange wa klabu bingwa Ulaya.
Wachezaji hao walijumuika katika kumbi moja na mwanamuziki Rihanna kutoka nchini Marekani ambaye yeye alikua ameenda kwa ajili ya maonesho ya mavazi na kupelekea kujumuika katika kumbi hiyo ya starehe ya usiku.


Ambapo kwa upande wa wachezaji hao wawili klabu yao ilikua inasafiri kesho yake wakiwa wanaelekea nchini Hispania kukabiriana na wababe wa nchini Hispania yani klabu ya Barcelona katika kombe la klabu bingwa ulaya na kupelekea kupokea kichapo kizito cha goli 6-1.


Powered by Blogger.