Kisa Future, Black Chyna adaiwa kuchanganyikiwa juu ya jambo hili


Zikiwa ni wiki kadhaa tu zimepita baada ya mwanadada anayefanya vyema kwenye game la Hip Hop duniani, Nick Minaj kuweka wazi juu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Meek Mill imevuja kuwa mwanadada huyo kwa sasa yupo karibu zaidi na rapa Future. 

Kwa mujibu wa TMZ imedai kuwa, chanzo cha karibu na rapa huyo, ukaribu wa Future na Minaj si wa kazi tu bali wapo katika uhusiano wa mapenzi jambo ambalo limemchukiza Black Chyna ambaye kwa sasa yupo ‘single’ baada ya kuachana na Rob Kardashian.

 

“Unajua Chyna alisema atafanya lolote liwezekanalo kumpata Future, sasa ukaribu wa Future na Minaj umemchanganya Chyna aliyeapa kuwatenganisha. Hata hivyo, Future hampendi Black Chyna aliyeonyesha hisia zake kwake waziwazi anampenda Minaj,” kilisema chanzo hicho.
Powered by Blogger.