KATIBU WA YANGA AZUNGUMZIA KUHUSU MCHEZAJI KUDAI MISHAHARA YAKEKatibu Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Charles Boniface Mkwassa amekiri klabu yake kudaiwa na mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Togo, Vicent Bossou.

Mlinzi huyo wa kati ilidaiwa ni mgonjwa wa nyonga ndiyo maana hakupangwa katika mchezo wa kichapo cha 2-1 kutoka kwa Simba SC siku ya Jumamosi iliyopita, lakini ukweli mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Togo aligomea mchezo huo kwa madai ya kudai mishahara yake ya miezi minne.

Nachofahamu mimi ni kwamba kuna mishahara ya mwezi wa nane ambayo ilicheleweshwa, si kwa Bossou tu ni timu nzima. Mshahara wa  mwezi wa 12 zikiwa zimebaki siku kumi kila mchezaji aliandikiwa cheki, wakalipwa pamoja na mshahara wa mwezi wa kwanza,” anasema  Mkwassa.

Kupitia Ukurasa wa mtandao wake wa kijamii Bossou aliweka wazi kuwa hajalipwa mshahara wa miezi minne sasa na kuutaka uongozi wake kumlipa haraka.
  
“Sasa wakati cheki zinatoka, Bossou alikuwa alikuwa kwenye mashindano AFCON kule Gabon na yule mtoa cheki hakumkabidhi mtu yeyote cheki ya mtu mwingine hadi muhusika mwenyewe awepo kwa hiyo cheki ya Bossou ilirudi ofisini.”
“Alivyorejea tulimwambia afuatilie cheki yake lakini hakwenda na tumejaribu kufuatilia tumeona kuna matatizo kidogo. Mshahara wa mwezi wa pili kila mchezaji bado hajapokea kama unavyojua timu yetu ina matatizo kidogo kwa mwenyekiti hivyo mambo mengi yamesimama.”
Powered by Blogger.