Kabla Ya Kuwa Mwanamuziki Bora Wa Kike Afrika Yemi Alade Aliwahi Kupita Huku

Jina lake halisi ni Yemi Eberechi Alade moja kati ya wasanii wa kike wanaofanya poa kwenye biashara ya muziki.

Yemi Alade alizaliwa Machi, 13 mwaka 1989 (Hivyo leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa), akiwa ni mtoto wa tano kati ya watoto saba kwenye familia ya baba yake James Alade. Yemi Alade ni miongoni mwa wanamuziki wasomi akiwa na Degree ya "Jiografia" aliyoipata Chuo kikuu Cha Lagos Nigeria.

Kabla ya kuwa Yemi Alade ambae mimi na wewe tumemjua kupitia ngoma kama Na Gode, Johnny Kissing na zingine Yemi amewahi kuwepo kwenye kundi la muziki la wasichana la "Not Spices" Nyota yake ilianza kung'aa mwaka 2009 aliposhinda kwenye mashindano ya "Peak Talent Show"  ya huko Nigeria, Baadae akachia wimbo wake wa kwanza "Fimisile" chini ya "Jus' Kiddin Label" lakini umaarufu wake ulikua zaidi baada ya kuachia ngoma yake "Johnny" ambayo ilitoka October 14, 2013 baada ya kupata dili la kusign na Effyzzie Music Group.
Kwa kukuongezea tu, Video ya wimbo Johnny ndio video ya msanii wa kiafrika inayoongozwa kwa kutazamwa zaidi mtandaoni mpaka sasa imeshagonga zaidi ya views milioni 63 youtube.

Muziki anaoufanya umempa dili nyingine kama kuonekana kwenye kurasa za mbele za majarida mbalimbali , kuhudhuria na kufanya shows kwenye matamasha makubwa ndani na nje ya Nigeria ambayo yamemkutanisha na wasanii wengine wakubwa kama  Mary J. Blige, Shina Peters, M.I, Wizkid, Becca, May D, Waje and YemiSax.

Mpaka sasa Yemi Alade amefanikiwa kuingiza Albamu mbili sokoni ya kwanza ikiwa ni  King of Queens (2014) na Mama Afrika (2016)'
Yemi Alade anamiliki tuzo mbili za MTV Africa Music Awards zote za mwanamuziki bora wa kike mwaka 2015 na 2016.

Miongoni mwa nyimbo zake hizi ndizo zilifanikiwa kufanya vizuri zaidi:
  • "Tumbum" (November 2016)
  • "Want You" (July 2016)
  • "Africa (ft. Sauti Sol)" (July 2016)
  • "Kom Kom (ft. Flavour)" (May 2016)
  • "Ferrari" (March 2016)
  • "Koffi Anan" (Freestyle) (January 2016)
  • "Classic Girl Freestyle" (Jidenna's "Classic Man" cover) (2015)
  • "Na Gode" (July 2015)
  • "Johnny" (October 2013)
  • "Fimisile" (2009)Kwa sas Yemi Alade anatamba na video ya wimbo wake "Marry Me" ambao upo kwenye Albamu ya "Mama Afrika" 


Powered by Blogger.