Jay Moe Azima Tetesi Za Kumchana Izzo Bizness Kwenye 'Nisaidie Kushare'Rapa Juma Mohamed Mchopanga a.k.a Jay Moe anayefanya poa na ngoma yake mpya kabisa inayokwenda jina 'NISAIDIE KUSHARE' ameondoa utata wenye mtazamo wa kuwa katika wimbo wake mpya kuna msanii wenzake amemchana.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio amekataa tetesi za kuwa alimchana Izzo Business hasa kile kipande cha “tunashare tu mapics kumbe track yenyewe sio” na kutmaja Izzo kuwa mmoja ya wasanii ambao anaheshimiana nao na wamemsupport sana kwenye kazi yake hii mpya.

“No…no…no…no siwezi Izzo ni mwanangu na  big up sana kwake kwasababu hao ni katika watu pia ambao wameweza kupush mpaka sasa hivi watu wengi wakawa wanajua kuhusu hiyo kitu…ni mtu wangu wa karibu yeye akitoa kazi wala hahitaji kuniomba nimsaidie kushare  atashangaa tu” Alisema Jay Mo.

Jay Moe mpaka kuachia wimbo wake huu mpya wa NISAIDIE KUSHARE ameweka nafasi ya muda miezi tisa tangu aachie wimbo wake wa PESA YA MADAFU.
Powered by Blogger.