Irene Uwoya Aeleza Alivyoshuhudia Ajali Mbaya Masaki

  
Mwanadada Irene Uwoya ambaye anafanya poa kwenye tasnia ya filamu Bongo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameeleza jinsi alivyoshuhudia dereva wa bodaboda akigongwa na gari na dereva inayedaiwa kuwa ni Mzungu, na kuachwa barabarani kwa muda mrefu, mpaka pale msanii huyo alipoamua kumsaidia kwa kumkimbiza hospitali.

Uwoya ameeleza kwamba jana majira ya usiku, akiwa anarejea nyumbani kwake ndani ya gari lake, akiwa anaendeshwa na dereva wake, walishuhudia ajali mbaya ambapo dereva huyo wa bodaboda, alikuwa amelala barabarani, damu nyingi zikimtoka huku akiugulia maumivu makali.

Msanii huyo akaendelea kueleza kwamba, ilibidi wasimame eneo hilo ambapo waliwakuta askari wakiwa ndani ya gari lao. Dereva wa bodaboda anayetajwa kufariki kwenye ajali hiyo

“Nikawauliza mbona huyu mtu anakufa mnamuangalia? Wakasema sisi tufanyeje wakati hakuna gari la kumbeba? Nikawaambia gari si hilo? Wakasema hapana hili haliwezi. Nikawaambia watu wampakie kwenye gari yangu… Nataka kuondoka wakaniambia nikachukue PF3 kwanza ndiyo niende…” aliandika Uwoya.

Akaendelea kueleza kwamba walipofika Hospitali ya Mwananyamala kwa kutumia gari la Uwoya, nako walichelewa sana kupata huduma. Hata baadaye kijana huyo alipoanza kuhudumiwa, tayari hali yake ilishakuwa mbaya, baadaye ndugu zake wakawasili ambapo walishirikiana kumhamishia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikopoteza maisha kesho yake.

“Leo asubuhi napiga simu kwa ndugu wa mgonjwa naaambiwa kafariki… Dah roho imeniuma sana haijawahi kutokea… Ila nitahakikisha haki inatendeka! Kweli watu wanashida jamani jamani usiombeee… Jana nimejifunza mengi… Daaah sisemi sana ila Mungu anajua. R. I. P brother,” aliandika Uwoya.
Powered by Blogger.