Idadi Ya Samaki zanzibar yazidi kupungua kutokana na hiliWaziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Zanzibar HAMAD RASHID MOHAMED amesema matumizi ya baruti, bunduki na mikuki bado yanaendelea kutumiwa na wavuvi wasio waadilifu kisiwani Zanzibar.
Habari zinasema vitendo hivyo vimefanya idadi ya samaki katika bahari ya eneo la Zanzibar ipungue.
Bw Hamad Rashid Mohamed amesema kwamba Wizara yake imeanza kufanya uchunguzi kuhusu uvuvi haramu, ambao ni tishio kubwa kwa sekta ya uvuvi ya Zanzibar  inayoajiri watu wengi wa Zanzibar.
Idadi ya wavuvi wa Zanzbiar inakadiriwa kuwa 34,500. Baadhi ya wavuvi wamelalamika kuwa uvuvi wa kutumia bunduki na mikuki umekuwa ukitumika kwa kipindi cha miaka miatatu sasa, kinyume na Sheria ya Uvuvi ya Zanzibar ya mwaka 2010.
Powered by Blogger.