Ice Boy afunguka juu ya ngoma yake mpya ‘Binadamu’ adai haihusiani na Young Killer ila....Rapper Ice Boy, ambae kwa sasa anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo “Binadamu”, akiwa amemshirikisha Mwanadada Nandy. Katika mahojiano wiki hii na GlobalTv, Ice Boy amefunguka vitu vingi ikiwemo safari yake alivyoanza muziki pamoja na sababu za kutunga kwa single yake ya sasa ‘Binadamu’.

Ice Boy alisema sababu zilizomsukuma mpaka kuandika single yake mpya ‘Binadamu’kwa maneno yake binafsi alidai "Hii ngoma inagusa watu wengi, wale wote wanao-struggle kila siku".

Aliendelea kuiongelea ngoma hiyo akisema "Binadamu’ imebase sana kwenye maisha yangu ya ukweli, inagusa karibia asilimia sabini ya maisha yangu mimi, hustle zangu, mishemishe, jinsi watu walivyonizingua na kunikunjia nisifike sehemu. Hii ngoma inagusa pia maisha ya watafutaji wengi wanao-struggle na maisha kila siku".
 
 
Mbali na hayo kumekuwa na tetesi kuwa ngoma hii kwa upande mmoja imemlenga msanii wa Hip Hop Young Killer, Ice Boy alilizungumzia hilo kwa kudai "Sitaki kumuongelea mchizi, nimesema hii ngoma inahusu maisha yangu so kama aliwahi kunikunjia basi itakuwa inamhusu" Ice Boy.

-GlobalTv 
Powered by Blogger.