Humprey Polepole Afunguka juu ya Mafao ya Marehemu Captain John Komba


Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kitaifa, Humphrey PolePole amefunguka kuhusu kilichojiri wiki iliyopita ambapo Mke wa Marehemu Captain John Komba, Salome Komba aliweza kuhojiwa na kumuomba Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk John Magufuli amsaidie ili aweze kulipwa ‘Mafao’ na ‘Stahiki’ za Mumewe.

Katika Mahojiano Jumanne hii Mhe. Humphrey PolePole alifunguka na kudai "Chama cha Mapinduzi ni chama kikubwa na watu wanapenda taarifa zetu. Hatupendi kujadili taarifa zetu barabarani, ila kiutaratibu Mama Komba anapaswa kufika Ofisini ili kujadili kuhusu mafao ya Marehemu Komba na kujadili mambo hayo kiustarabu".

Aliendelea, "Mambo yote nyeti kuhusu stahiki za mtu ni jambo binafsi,na siwezi kuanza kuyajadili nje ya ofisi aswa pesa za mtu. Namshauri Mama Komba afate utaratibu maana anafahamu utaratibu wa CCM. Afike ofisini tumsikilize ili tutoe majibu kwa wakati”. ALieleza hayo Humprey Polepole kwenye kipindi cha Maisha Mseto.
Powered by Blogger.