Haya hapa Maneno ya Nikki wa Pili kwa wasanii wa Bongo Fleva


Rapa Nikki wa Pili kutoka Weusi Kampuni huwa haishiwi ushauri pale anapoona kuna jambo linalofaa kuigwa kama sio kujifunza na hii yote ni kutokana na utashi na uelewa wake ukijumlisha na elimu pia aliyonayo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameona ni kheri akawashauri pia wasanii wa muziki kuwa kwa sasa ni vyema kufanya muziki wanaoupenda mashabiki kwa kuwasikiliza hao na sio kuwasikiliza wakosoaji.Kama unataka kufanya biashara ya muziki wasikilize zaidi wateja, kuliko wakosoaji“Ameandika Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Powered by Blogger.